Dk. Tulia Akson awaonya wanachuo wa vyuo wa kike .

DK TULIA

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia  Akson amewataka wanachuo wa vyuo wa kike hapa nchini kuwa na ujasiri wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza badala ya kuuza miili yao na kupunguza thamani ya utu yao.

Naibu huyo ametoa kauli hiyo  mjini dodoma wakati akizungumza na na wanachama wa kike wa shirikisho la vyuo vikuu mjni Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya miaka 40 ya chama cha CCM kwa jumuiya wa wanawake wa CCM Taifa UWT.

 Hata hivyo maadhimisho hayo ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM) mwaka 1977, yanatarajiwa kufanyika kitaifa feb 5 mwaka huu  kitaifa mjini Dodoma.

 Aidha Dk Tulia amesema kuwa wanachuo hao kudhamini utu wao badala ya kujingiza kwenye masuala ya kuuza miili yao.

Amesema kuwa wao kama wanawake wanaotaka kwenda mbele zaidi ya hapo walipo kuwa viongozi wa kubwa wanatakiwa kuthamini utu wao badala ya kujingiza kwenye masuala ya rushwa ya ngono.

kwa upande wao baadhi ya wanavyuo walioshiriki maadhimisho hayo wamewasihi wanavyuo wa kike wenzao kutojiingiza katika vitendo kuuza miili yao kutokana na changamoto wanazozipata.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa ofisi ya chma cha mapinduzi ccm ambao yamewakutanisha wanachama wa kike wa shirikisho hilo kutoka chuo cha mipango,St. John,chuo cha biashara na uchumi (CBE) na chuo kikuu cha dodoma (UDOM).

Imeandaliwa na Barnaba Kisengi

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments