Diego Costa asema Chelsea wanamchukulia kama ‘mhalifu’.

Diego Pc

Diego Costa amesema Chelsea wamekuwa wakimchukulia kama “mhalifu” na akathibitisha kwamba bado anataka kurejea Atletico Madrid.

Mshambuliaji huyo wa miaka 28 alichezea Chelsea mara ya mwisho fainali ya Kombe la FA mwezi Mei na mwezi Juni alitumiwa ujumbe wa simu na meneja Antonio Conte kumfahamisha kwamba hakuwa kwenye mipango yake ya msimu ulioanza siku chache zilizopita.

Costa amesema sasa klabu hiyo inamshurutisha kurejea akafanye mazoezi na wachezaji wa akiba.

“Ni kwa nini hawataki kuniacha niondoke iwapo hawanitaki?” aliambia Daily Mail.

“Lazima nifanye yale inanibidi kuyafanya. Lazima nifikirie kuhsuu maslahi yangu. Nimekuwa mvulana mzuri hapa na nilijaribu kufanya kila kitu sawa. Mapenzi yangu ni kwenda Atletico.”

Costa anaamini kwamba meneja Antonio Conte ndiye anayemchongea.

“Januari, mambo yalifanyika kati yangu na kocha. Nilikuwa nimekaribia sana kutia saini mkataba mpya lakini akasimamisha hilo. Nashuku meneja alihusika. Aliomba hilo lifanyike.

  • #BBC SWAHILI
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments