DAWASCO wana watu maalum wa kusimamia na kufatilia miundombinu

Shirika la maji safi DAR ES SALAAM (DA WASCO) limeamua kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa ukamilifu.

 

 

Akizungumza na  na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM ,Mhandisi   TYSON MKINDI amesema DAWASCO wana watu maalum wa kusimamia na kufatilia miundombinu yote pindi inapotokea hitilafu hata kama ni usiku.

 

Mhandisi MKINDI amesema sasa wapomaeneo ya tupo hapa maeneo ya SURVEY ,DAR ES SALAAM, muda huu wa saa 6 usiku wanaendelea kurekebisha bomba kuu la maji linaloelekea mjini,maeneo ya MANZESE na MAGOMENI.

 

Aidha Mhandisi MKINDI amesema ukarabati wa bomba hilo unatokana na hitilafu iliyojitokeza katika maungio ya bomba na sehemu zinazoshikilia bomba hilo.

 

Amesema mpaka kufikia jioni ya leo hali itakuwa nzuri na maji yataanza kutoka maeneo yote

Comments

comments