Damiani Mguya kusitishiwa kwa muda leseni ya Uuguzi na Ukunga.

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeagiza Baraza la Uuguzi na Ukunga mkoa wa TABORA kusitisha kwa muda leseni ya Uuguzi na Ukunga  kwa muuguzi DAMIANI MGUYA kwa kuvunja kifungu cha 13(2) cha THE NURSING AND MIDWIFERY ACT 2010.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Idara Kuu Afya BW.NSACHRIS MWAMWAJA imesema BW.DAMIAN MGUYA amekiuka maadili kwa kumpatia dawa ya usingizi mgonjwa na kumlewesha kasha kumbaka.

Aidha Wizara imelaani kitendo hicho kwa kuwa kimelenga kuidhalilisha taaluma hiyo hivyo imewakumbusha  watumishi wote wa sekta ya afya nchini kuzingatia maadili ya taaluma zao wakati wowote.

Mwanzoni mwa wiki hii muuguzi DAMIAN MGUYA alimuwekea dawa ya usingizi iliyomlewesha binti huyo na kasha kumbaka akiwa katika chumba maalum cha kusubiri huduma.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments