Cristiano Ronaldo kupata uwanja wa ndege.

RONALDO

Cristiano Ronaldo alifunga bao kwenye mechi iliyochezewa katika kisiwa alikozaliwa cha Madeira, siku moja kabla ya uwanja wa ndege katika eneo hilo kupewa jina lake.

Ureno hata hivyo, walitupa uongozi wa mabao mawili na mwishowe wakalazwa 3-2 na Sweden.

Ureno walikuwa wanaongoza kupitia bao la 71 la Ronaldo katika michuano ya kimataifa, pamoja na bao la kujifunga na Andreas Granqvist.

Lakini Viktor Claesson alifunga mawili naye Cavaco Cancelo kajifunga dakika za mwisho mwisho na kuwapa Sweden ushindi.

Ronaldo anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya kuupa uwanja huo jina lake Jumatano.

#SIBUKAMEDIA

#BBC SWAHILI

Comments

comments

Random Posts