Chelsea v Man Utd: Jose Mourinho awaambia Blues bado anaongoza Chelsea.

SPORTSS

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewaambia mashabiki wa Chelsea kwamba yeye bado ni “Number One” (Nambari Moja) baada yake kuzomewa wakati wa mechi ambayo mabingwa hao watetezi wa Kombe la FA walilazwa 1-0 uwanjani wa Stamford Bridge Jumatatu.

Mourinho, ambaye alifutwa kazi mara mbili na Chelsea, aliitwa ‘Yuda’ na mashabiki wakati wa mechi hiyo.

Hata hivyo, aliwajibu kwa kuwaelekezea vidole vitatu, ishara ya mataji matatu ya ligi aliyoyashinda akiwa na klabu hiyo.

Wachezaji wa Chelsea akiwemo N'Golo Kante wakisherehekea bao.

Wachezaji wa Chelsea akiwemo N’Golo Kante wakisherehekea bao.

Alisema baadaye: “Hadi wampate meneja ambaye atawashindia mataji manne ya Ligi ya Premia, mimi bado ni nambari moja.

#BBC SWAHILI

SIBUKAMEDIA

Comments

comments