Chama cha wanawake (TAMWA) kimeiasa jamii kuwalea watoto kwenye maadili mema.

IMG_4184

 

Chama cha wanahabari wanawake Tanzania(TAMWA) kimeiasa jamii kuwalea watoto katika maadili mema kuwajali na kuwapenda ili baadae waweze kujiepusha na vitendo vya kikatili.

Akizungumza afisa mradi wa Tamwa Bi Godfrida Jola kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji        wakati wa mkutano wa TAMWA wa siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika  kuwa ni wajibu wa jamii kulinda haki za mtoto kwa kuhakikisha vitendo vya kikatili vinatokomezwa duniani na kupatiwa mahitaji yote stahiki.

IMG_4269

Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009  sura namba 21 ambayo utekelezaji wake umeshaanza ni vema jamii kukidhi mikataba ya kimataifa na kikanda kuhusu haki na ustawi wa motto ambayo ilisainiwa na kuridhiwa sambamba na sera ya taifa ya maendeleo ya motto ya mwaka 2008.

Nae katibu mkuu mstaafu wa African Inland Church Tanzania Bw. Lucas Singili akiongea kwa niaba ya CCT amesema kuwa leo ni siku nzuri ya kukumbuka historia wajibu wa kila mmoja wetu katika kuhakikisha maisha bora na salama kwa kila mtoto wa Tanzania na Afrika ili kukua na kustawi kiafya na kiakili.

Bw. Singili ametoa wito kwa jamii kuzidi kuelimishwa katika dini ili kuishi katika misingi mema ya dini itakayosaidia kuondoa ukatili dhidi ya mtoto.

Kwa upande wake Shekh Shomari Mchongoma kutoka Baraza la waislamu Tanzania (Bakwata) amesema kuwa ni wajibu kwa wazazi kuwalea na kuwatunza watoto pamoja na kuwajenga kiimani ili waweze kuwa na imani hapo baadae jambo litakaloondoa ukatili kwa watoto.

IMG_4240

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kuanzia tarehe 1 juni kila mwaka ambapo hufikia kilele siku ya tarehe 16 juni ambapo  kauli mbiu ni “Migogoro na michafuko ya afrika tuulinde haki za watoto

 

Mwandishi : Tuse Kasambala.

 

 

Comments

comments

Random Posts