Chama cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA)

shida-20170224-WA0004

Chama cha wanasheria wanawake Tanzania(TAWLA) kimewakutanisha wadau mbalimbali jijini Dar es salaam ili kujadili suala zima la madhara yatokanayo na mimba zinazotolewa kwa njia zisizo salama ambazo zimekuwa zikisababisha vifo katika uzazi.
Amesema hayo leo mwezeshaji katika mafunzo hayo ya TAWLA Bw. Pasiens Mapunda ambae ni mhadhiri mwandamizi afya ya jamii kutoka chuo cha mtakafu Hubert amesema kuwa utoaji huo wa mimba kwa njia zisizo salama na wakati wa kujifungua umekuwa ukisababisha wanawake kutoka damu kwa wingi na kuchangia vifo hivo kwa asilimia 13 hadi 15 ya vifo nchini.

pumbavu zake
Ameongeza kuwa hali hii imekuwa ikisababishwa na upatikanaji wa mimba usiotarajiwa kutokana na mazingira ya ukatili wa kijinsia ambapo wanawake wengi hudhalilishwa kwa kubakwa na mzazi,ndugu, vichaa au majambazi na kujikuta wakilazimisha kutoa kwa usiri bila kuzingatia usalama katika utoaji wa mimba hizo.
Bw.Mapunda amesema kuwa kulingana na sheria ya nchi hii imekuwa suala gumu kwa wanawake kujitokeza katika vituo vya afya pindi hali inapobadilika mara baada ya zoezi la utoaji mimba usio salama na hivyo kujikuta wakipoteza maisha yao.
Amebainisha kuwa sheria ya Tanzania inasema kuwa hairuhusiwi kutoa mimba isipokuwa inapotokea dharura ya kuokoa maisha ya mama ambapo sheria imesema kuwa kutoa mimba ni kosa na atakaeshikwa mimba adhabu yake ni miaka 14jela,atakayesaidia kutoa mimba adhabu yake ni miaka7 jela na miaka mitatu kwa atakayesaidia vifaa.
Aidha amesema kuwa ipo haja kwa serikali kuangalia upya suala zima la mimba zisizotarajiwa kwa wanawake hapa nchini kwa kuwa kimataifa suala hilo limekubaliwa kisheria kutolewa kwa mimba zisizokubalika zilizopatikana kwa kubakwa.
Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau kutoka wizara ya sheria, wizara ya afya na wadau wa masuala ya afya na uzazi salama.

# SIBUKA MEDIA

#Imeandaliwa na Tuse Kasambala

Comments

comments

Random Posts