Chama cha wananchi (CUF) kimetolea ufafanuzi maamuzi ya Mahakama Kuu.

Chama cha wananchi (CUF) kimetolea ufafanuzi maamuzi  ya Mahakama Kuu  kuhusu shauri la msingi namba 143/2017 lililofunguliwa na wabunge 8 na madiwani 2 wa manispaa za UBUNGO na TEMEKE ya kupinga kuvuliwa uanachama na zuio la muda wa kusikiliza shauri namba 447/2017 .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM, Mkurugenzi wa Habari BW. MBARARA MAHARAGANDE amesema wamepokea maamuzi  hayo ambayo ni sahihi kwa mujibu wa maoni ya jaji  kisheria, na si hujuma dhidi ya Haki kama baadhi ya watu wasiojua taratibu na misingi ya sheria.

 MAHARAGANDE amesema hakuna maamuzi yoyote mpaka sasa yaliyotolewa na Mahakama Kuu katika kadhia hii inayoendelea zaidi ya Kuzuia Ruzuku isitolewe kwa LIPUMBA na genge lake na hili la kuondoa maombi madogo yaliyowasilishwa.

 Amesema kuwa pingamizi ni hoja za kisheria pekee (pure points of law) kati ya hoja 4 zilizowasilishwa hoja 3 zimekataliwa na moja kukubaliwa ambayo iliyohusiana na matumizi ya sheria za uingereza (Common Law)  section  2(3) ya JALA kifungu ambacho kwa mtazamo/maoniya Jaji hakiipi mamlaka ya kisheria Mahakama kusikiliza maombi hayo.

Hata hivyo amesema wabunge wa CUF tayari wametayarisha nyaraka na kusainiwa pamoja na marekebisho yote ya msingi na ya lazima yaliyopaswa kuingizwa ikiwemo kuwajumuisha katika shauri hilo Wakurugenzi wa Manispaa za UBUNGO na TEMEKE ambao wanahusika kutokana na Madiwani katika halmashauri zao kuathiriwa na maamuzi ya LIPUMBA.

 Septemba 24,2016 Chama cha wananchi CUF kilifungua kesi ya  Mashauri 6 ya Msingi Pamoja na mashauri madogo likiwemo la wabunge 8 na madiwani 2 kuvuliwa uanachama.

  • Mwandishi : Tuse Kasambala.
  • Mhaririri : Amina Chekanae.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts