Chama cha wananchi CUF kimesema hakiwatambui wabunge wanane walioapishwa jana mkoani DODOMA.

Chama cha wananchi CUF upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim SEIF SHARIF HAMAD kimesema hakiwatambui wabunge wanane walioapishwa jana mkoani DODOMA.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo Naibu Kaimu Mkurugenzi wa Habari Bw.MBARARA MAHARAGANDE amesema kitendo cha kuapishwa kwa wafuasi hao kimefanyika  haraka bila kuzingatia utaratibu.

MBARARA amesema kuwa michakato  hiyo ya kuapishwa kwa wabunge hao  wapya ilipaswa kusubiri hatma ya mahakama kabla ya kufanya hivyo na kusema kuwa spika anapaswa kujitathmini kwa kuwa amepoteza sifa.

Nae  wakili wa mahakama na mwanachama wa CUF  HASHIM MZIRAY amesema jamuhuri ya muungano wa Tanzania inaongozwa na katiba hivyo maamuzi ya kuondolewa yanaweza kukatiwa rufaa.

Mmoja wa wabunge waliovuliwa uanachama BI. RIZIKI SHAHARI amesema kuwa wataendelea kupigania  kupigania demokrasia na kuzitaka taasisi za serikali zisitumike kuhujumu vyama vya upinzani.

Chama cha wananchi (CUF) kimekuwapo katika mgogoro wa muda mrefu baina ya upande wa Katibu mkuu Maalim SEIF SHARIF HAMAD na Profesa IBRAHIM LIPUMBA ambapo umesababisha kufunguliwa kwa mashauri mbalimbali yanayoendelea mahakamani.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments