Chama cha wananchi CUF kimeelezwa kusikitishwa na matamko mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa chama cha chadema na kuingilia kati mgogoro wao kwa nia ya kuifuta CUF upande wa Tanzania bara .

CT79ZQlWIAA6GBS

Chama cha wananchi CUF kimeelezwa kusikitishwa na  matamko mbalimbali yanayotolewa na viongozi  wa chama cha chadema na kuingilia kati mgogoro wao kwa nia ya kuifuta CUF upande wa Tanzania bara .

Hayo yamesemwa leo jijini DAR ES SALAAM na Kaimu  Katibu Mkuu BI. MAGDALENA SAKAYA alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari amekilaumu chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) na viongozi wake kushirikiana na Katibu mkuu wa CUF  MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD.

Aidha Sakaya amesema mipango hiyo ni pamoja na kuvamia ofisi ambapo sasa wameenda mbali zaidi na kuamua kujitokeza kwenye kesi zilizofunguliwa na washirika wao dhidi ya viongozi wa CUF.

Hata hivyo amekiomba chama cha CHADEMA kujikita katika kutafuta sababu za wanachama na viongozi wao kuhama katika chama chao na kujiunga na chama cha CCM na si kuingilia kati mgogoro wa CUF ambao kimsingi hauwahusu.

Amesema kuwa uwepo wa viongozi wa CHADEMA mahakamani katika kesi zilizofunguliwa  ni ushahidi tosha wa maazimio ya vikao vyao kuwa wanahusika na mgogoro unaoendelea ndani ya  CUF.

Sakaya amewakata wanachama wa CUF kuendelea kukilinda chama kwa mujibu wa katiba ya chama .

 

#Imeandaliwa na Tuse Kasambala.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments