Chama cha wananchi cuf kimeeleza kushtushwa na muendelezo wa hujuma.

CUF

Chama cha wananchi cuf kimeeleza kushtushwa na muendelezo wa hujuma zinazofanywa na msajili wa vyama vya siasa nchini jaji Fransic Mutungi dhidi ya cuf kwa kutumia wakala wa usajili (RITA)

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf kuwa hujuma hizo zinahusisha mbinu chafu za kughushi nyaraka ambazo kwa mujibu wa Maalim Seif rejea kikao kilichofanyika tarehe 9 April 2017 zimesema kuwa lengo la Mutungi ni kumsaidia Profesa Lipumba kuhakikisha bodi ya wadhamini feki inasajiliwa.

Amesema kuwa bodi hiyo ambayo iliandaliwa kuchukua nafasi ya bodi halali wadhamini ya cuf kwakuwa chama cha wananchi ni kikwazo katika kufanikisha mipango yao haramu ya kufungua akaunti mpya ya benki ili kuwezesha wizi wa ruzuku ya chama.

Aidha maalim Seif amebainisha kuwapo kwa taarifa kuwa  afisa mtendaji mkuu wa RITA amepata shinikizo kubwa la kusajili wajumbe feki wa bodi ya wadhamini ya cuf kwa kutumia majina yaliyowasilishwa na pro.Lipumba ili kuhujumu majina halali yaliyopitishwa na baraza kuu la uongozi la Taifa ya kikao kilichofanyika tarehe 19 march huko Zanzibar.

Ameongeza kusema kitendo cha RITA kukataa kumpa nafasi maalim Seif ambaye aliandika barua tatu machi 31 na june 6 2017  ya kukutana na kabidhi wasihi mkuu wa RITA na wakati huo ikimpa nafasi Lipumba kimedhihirisha kuwa RITA wamejiunga na jaji mutungi jambo ambalo limepelekea cuf kuadhimia kufungua kesi dhidi ya RITA kwa kukiuka sheria.

Chama cha cuf kimewakutanisha wabunge 42,madiwani pamoja na wanachama ili kutoa taarifa kwa umma dhidi ya maadhimio ya kusimamisha kesi nyingine zote hadi shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA litakapoamuliwa.  

  • Mwandishi : Tuse Kasambala
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments