vlcsnap-2016-07-20-17h08m25s216

Chama cha NCCR-MAGEUZI chamvua uwanachama Bi. Leticia Mosore

vlcsnap-2016-07-20-17h08m25s216

Chama cha NCCR-MAGEUZI kimemsimamisha na kumvua uwanachama makamu mwenyekiti taifa wa chama hicho bara Bi. Leticia Mosore kwa makosa mbalimbali aliyoyatenda wakati wa uchaguzi mkuu 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mwenyekiti wa chama hicho taifa bwana James Mbatia amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha halmashauri kuu ya taifa kukaa ambapo bi. Leticia alipatikana na hatia nyingi ikiwamo kujihusisha na migogoro ndani ya chama na kutoa tuhuma dhidi ya kiongozi wa chama au mwanachama nje ya utaratibu huku akikashifu uongozi wa chama.

Akizungumza kuhusu umoja wa katiba  ya wananchi bwana Mbatia amesema kuwa  UKAWA ni zaidi ya vyama vya siasa hivyo NCCR – MAGEUZI itaendelea kusimama imara kuhakikisha kuwa taifa linapata katiba mpya inayotokana na wananchi kama yalivyokua malengo ya umoja huo.

Comments

comments