Chama Cha Kutetea Abiria Tanzania Kimeomba Serikali kuongeza idadi ya daladala.

Daladala

Chama Cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) Kimeomba Serikali kuongeza  idadi ya daladala ili kupunguza adha ya usafiri kwa abiria.

Hayo yamebainishwa na Mratibu Mtendaji mkuu   Chama cha kutetea  Abiria Tanzania (CHAKUA)BW. MONDAY LIKWEPA wakati akizungumzia changamoto wanazozipata abiria katika safari zao,Huku jiji la  Dar es salaam likikadiriwa kuwa na wakazi milioni tano na nusu wenye changamoto nyingi za kiusafiri.

Hata hivyo BW.LIKWEPA amewataka,Madereva na Makondakta wa daladala wanaopenda kukatisha ruti na kupandisha nauli kiholela waache  kwani kufanya hivyo ni wizi na watashughulikiwa endapo wakibainika.

Aidha BW.LIKWEPA ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kutoza kodi kwa mwaka katika vyombo kama baiskeli,maguta na mikokoteni kama ilivyokua zamani ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kukuza utamaduni wa taifa,michezo,sanaa na Habari.

  • Mwandishi : Glady Joseph.
  • Mhariri : Amina Chekanae.
  • #SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments