Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetowa tamko juu ya kukamatwa kwa mwanasheria wa chama hicho BW.TUNDU LISSU

tundu-lissu-300x200

Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kimetowa tamko juu ya kukamatwa kwa mwanasheria wa chama hicho BW.TUNDU LISSU kwa madai ya kumkashifu Rais na uchochezi kuhusu kuzuiliwa kwa ndege ya serikali ya bombardier.

Akizungumza na sibuka fm mkuu wa idara ya habari na mawasiliano {CHADEMA} BW. TUMAINI MAKENE amesema inadaiwa makosa hayo yamefanyika kwenye mkutano na wandishi wa habari agosti 18 mwaka huu.

Aidha BW MAKENE ameongeza kuwa chama kinaendelea kusisitiza kuwa serikali bado inao wajibu wa kujibu hoja za msingi zilizotolewa na Chama kupitia tamko lililosomwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama BW.LISSU kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania huko nchini CANADA kwa sababu ya deni tunalodaiwa kama nchi la shilingi bil. 87.

Hata hivyo CHADEMA kimeshatoa maelekezo kwa wanasheria wa chama kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria iwapo Jeshi la Polisi halitampeleka mbele ya mahakama LISSU ndani ya muda unaoagizwa na sheria za nchi yetu.

  • Mwandishi : Anne Julius.
  • Mhariri : Amina Chekanae.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments