Chama cha demokrasia na maendeleo {CHADEMA } kimesema hali ya mwanasheria TUNDU LISSU inaendelea kuimarika na kuwaomba watanzania kuendelea kumchangia.

Mbunge wa Singida

Chama cha demokrasia na maendeleo  {CHADEMA } kimesema hali ya mwanasheria TUNDU LISSU inaendelea kuimarika na kuwaomba watanzania kuendelea kumchangia.

Akizungumza na wanahabari Katibu mkuu wa CHADEMA DKT. VICENT MASHINJI amesema mwanasheria LISSU ameshafanyiwa upasuaji mara 3 na kwamba bado pesa zinahitajika kwa ajili ya matibabu.

Aidha ameongeza kuwa safari ya matibabu ya BW.LISSU bado ni ndefu lakini wao kama chama watahakikisha wanatumia rasilimali zao zote katika matibabu ya mpambanaji wa haki za watu Nchini.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments