Chama cha Alliance for Democratic Change kimempongeza Rais DK.JOHN POMBE MAGUFUL

DAR ES SALAAM:
Chama cha Alliance for Democratic Change kimempongeza Rais DK.JOHN POMBE MAGUFULI kwa juhudi za kuzuia rasilimali za nchi zisiporwe na wachache wakiwemo wageni.
Hayo yamesemwa jijini DAR ES SALAAM na Katibu mkuu BW. DOYO HASSAN DOYOkatika mkutano wa wanahabari na kuongeza kuwa chama cha ADC kinamuunga mkono Rais Magufuli na serikali yake kwa juhudi kubwa za kuwaokoa watanzania pamoja na rasilimali zao.
BW.DOYO amesema kuwa chama hicho kinatarajia kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake tarehe 22 AGOSTI,2017 ambapo siku hiyo watafanya ziara za kijamii sambamba na kufungua matawi mapya ili kuendelea kuimarisha chama.
Akizungumzia hali ya siasa nchini DOYO amesema si nzuri kwakuwa kumekuwa na ukosefu wa uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa hasa kwa upande wa vyama vya upinzani.
Pia wamekitaka chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuacha kuingilia mgogoro wa CUF wa njama za kumuondoa kwa nguvu mwenyekiti halali Profesa IBRAHIMU LIPUMBA
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa chama cha ADC Bi. QUEEN CUTHBERT SENDIGAamewataka wanasiasa kumuunga mkono Rais MAGUFULI kuhusu katazo la mwanafunzi mjamzito kutokuendelea na masomo kwani kuruhusu kuendelea na masomo ni kudidimiza kiwango cha elimu nchini.

#Imeandaliwa na Tuse Kasambala

# SIBUKA MEDIA

Comments

comments