Cameroon yanyakua ubingwa AFCON.

Cameroon

Timu ya Taifa ya Cameroon imeibuka bingwa wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa kuifunga Misri bao 2 kwa moja.

Bao la ushindi liliingizwa golini katika dakika ya 88.

Misri ambayo ilikuwa imenuia kushinda mashindano hayo na kuweka rekodi ya mshindi mara nane, ilikuwa ikiongoza katika kipindi cha kwanza.

NI mara ya tano kwa Cameroon kubeba kombe hilo ya mataifa ya Afrika na mara yake ya kwanza tangu mwaka 2002.

#SIBUKAMEDIA

#BBC SWAHILI

 

Comments

comments

Random Posts