David-Cameron-Getty-v3

Cameron afanya mkutano wa mwisho na mawaziri.

David-Cameron-Getty-v3

David Cameron ameongoza kikao chake cha mwisho cha baraza la mawaziri baada ya kuwa waziri mkuu wa Uingereza kwa miaka sita ambapo anampisha katika nafasi hiyo  waziri wa mambo ya ndani Theresa May kujiandaa kuunda serikali mpya baada ya kura ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Kuondoka madarakani kwa Cameron kumekuja mapema kuliko ilivyotarajiwa kufuatia mabadiliko ya ghafla katika kinyang’anyiro cha kumrithi ambapo naibu waziri wa nishati Andrea Leadsom alijitoa dakika za mwisho na kumuachia Theresa May kuibuka mshindi wa wazi katika chama hicho cha Conservative. Kesho waziri mkuu David Cameron atawasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia Elizabeth wa pili na kutoa nafasi kwa  Theresa May kuanza mara moja majukumu yake kama waziri mkuu mpya ikiwa ni pamoja na kuunda serikali.

Source: Dw

Comments

comments