BW. HUMPHREY POLEPOLE amekemea vikali mauaji yanayoendelea mkoani PWANI.

Humphrey-Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, BW HUMPHREY POLEPOLE amekemea vikali mauaji yanayoendelea mkoani PWANI.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM,POLEPOLE amesema kama chama kinachoongoza serikali wamejipanga na wanataka kuona mambo hayo yanakemewa vikali.

BW.POLEPOLE ameonyesha masikitiko yake kwa vyama vya upinzani kukaa kimya  huku wakitupia lawama serikali.

Wakati huo huo Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(CCM)umesema umeridhishwa na hatua stahiki anazozichukua Rais DKT.JOHN POMBE MAGUFULI kwa kuzingatia Ilani ya Chama.

Aidha Umoja huo umempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uzalendo wa hali ya juu alionao kwa Taifa.

Aidha umoja huo umemuomba Rais DKT.MAGUFULI kuwaweka pembeni wasaidizi wake wote ambao bado wanaonekana kuwa na kigugumizi katika kuwatumikia wananchi huku baadhi yao wakiona muhali kupambana na ufisadi.

Pia umoja huo unawataka wana CCM na watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais DKT.MAGUFULI na serikali yake katika mapambao dhidi ya vikundi vya rushwa,ufisadi na uzembe kwa baadhi ya watendaji ili kuleta maendeleo.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts