Bw. Boniface Jacob Akieleza mashtaka, Kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Mstahiki meya wa jimbo la UBUNGO (CHADEMA) BW.BONIFACE JACOB ameelezea mafanikio ya vielelezo vya mashtaka aliyopeleka kwa tume ya maadili kuhusu mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM BW.JACOB amesema kuwa machi 22  mwaka huu alipeleka rasmi mashtaka ya kumshtaki kiongozi huyo kughushi vyeti,kula  kiapo cha utii kwa raisi,matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kujipatia mali kwa njia zisizo sahihi.

Aidha pamoja na mashitaka hayo JACOB ameongeza kuwa  amewasilisha vielelezo  vya majina yake,vyeti na wanafunzi aliosoma nao.

Hata hivyo mstahiki meya ameipongeza tume ya maadili kwa kuonyesha mwanzo mzuri ambapo imetoa majibu ya barua iliyopelekwa kwa tume dhidi ya malalamiko hayo  na kero za mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM.

Mwandishi: Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments