BUNGE limesema kuwa hakuna jinsi yoyote kujitenga kwenye kushiriki maonesho ya wakulima Nanenane

BUNGE

BUNGE limesema kuwa hakuna jinsi yoyote ambayo muhimili huo unaweza kujitenga kwenye kushiriki maonesho ya wakulima Nanenane kwa kuwa sera na sheria za kilimo zinatungwa bungeni.

Ofisa habari wa Bunge,PATSON ASUMWISYE SOBHA amesema hayo alipokuwa akitoa maelezo ya shughuli za Bunge kwa Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,DKT.CHARLES TIZEBA wakati alipotembelea kwenye maonyesho ya  Nanenane yanayofanyika uwanja wa kilimo  NZUNGUNI DODOMA.

Kwa upande wake ZUHURA MTATIFIKOLO,kitengo cha habari za Bunge amesema maonesho ya nanenane ni chachu ya maendeleo kwa wakulima,wafugaji pamoja na wavuvi kwa kupata elimu ya sekta hizo.

Kwa upande wake Waziri wa Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi DKT.CHALERS TIZEBA amesema ni jambo jema kwa kila mwenye ujuzi na nafasi ya kujua jambo akatoa elimu kwa sekta hizo muhimu.

Amesema kuwa nchi ikiwa na mkakati wa kuelekea katika uchumi wa kati na wa Viwanda ni lazima wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi wakapatiwa elimu ya kutosha juu ya ufanyaji wa kazi zao badala ya kufanya kwa mazoea na bila kuwa na tija.

Amesema sekta ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi  zinatakiwa kupewa kipaumbele kwa lengo la kuwa na uzalishaji bora na wenye tija ili kulifikisha taifa katika uchumi wa kati na uchumi wa Viwanda.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts