Binti aliyetaka kujiua apata nafasi nyingine ya kuishi baada ya kupandikizwa sura

Haki miliki ya pichaFAMILY/MARTIN SCHOELLER
Image captionKatie alifanyiwa upandikizwaji wa sura yake mwezi mei mwaka 2017

Katie Stubblefield alikuwa na umri wa miaka 18 wakati alipopata majeraha makubwa baada ya kupigwa risasi.

Aliokolewa maisha yake hospitalini ingawa majeraha aliyoyapata yalimfanya msichana huyu maisha yake yabadilike na muonekano wa uso wake ulikuwa umebadilika karibu wote.

Kwa sasa msichana huyo ana umri wa miaka 22 na ameweza kuonyesha matokeo ya upandikizaji wa uso wake ulichukua miaka kadhaa katika jarida la ‘National Geographic’

Chapisho hili lilipata nafasi ya kipekee katika kilniki ya Ohio ambayo ilimfanyia upasuaji binti huyo wakati akiwa ana umri wa miaka 21.

National Geographic
Image captionJarida la National Geographic

Waandishi wa habari na wapiga picha walifuatilia upasuaji huo tangu maandalizi yanaanza mpaka wakati wa upasuaji ambao ulitumia muda wa saa 31.

Picha ya sura ya Katie ambayo ipo juu ya jarida hilo la mwezi wa septemba iliweza pia kusimuliwa katika Makala ya kwenye mtandao.

Mpaka sasa ni watu 40 tu ndio wameweza kubadilishwa muonekano wa sura zao.Mtu wa kwanza kufanyiwa upandikizaji huo ilikuwa mwaka 2010 na alifanyiwa na daktari kutoka Uhispania.

Kwa kuwa upasuaji huu bado unafahamika kama ni majaribio hivyo basi malipo yake hayapo kwenye bima nchini Marekani.

Upasuaji alioufanya Katie ulidhaminiwa na taasisi ya ‘Armed Forces’ambayo inataka kuboresha matibabu ya askari ambao watakuwa wamejeruhiwa katika vita.

Katie aliaminika kuwa ni mtu sahihi kufanyiwa jaribio hilo kutokana na majeraha aliyokuwa nayo pamoja na umri wake.

KatieHaki miliki ya pichaBENNINGDON FAMILY/MAGGIE STEBER/ NATIONAL GEOGRAPH
Image captionBibi yake Adrea akiangalia muonekano unaofanana na mjukuu wake katika uso wa Katie

Sura aliyopandikizwa Katie ilikuwa imetoka kwa Adrea Schneider mwenye umri wa miaka 31 aliyekufa kutokana na kutumia madawa ya kulevya kuzidi kiwango mwaka 2017.

Maamuzi ya kutolewa kwa uso wake ulitoka kwa bibi yake aitwaye Sandra Bennington ambaye alikuwa anafuatilia upasuaji wa Katie tangu alipomuona.

Katie anasema hawezi kukumbuka sana kuhusu wakati alipotaka kujaribu kujiua lakini familia inasema Katie alikuwa anasumbuliwa sana kifikra na mahusiano yake yalikuwa yameshindwa kuendelea na vilevile matatizo ya kiafya ambayo yalikuwa hayakomi wakati wote wa ukuaji wake kama kijana.

Majeraha ya risasi yaliweza kujeruhi sehemu kubwa ya uso wake ikiwa pamoja na pua ,paji la uso na muonekano wa mdomo.Katei alikuwa pia ana majeraha kwenye ubongo pamoja na macho.

Mississippi alihamishwa kwenda Tennessee kabla ya upasuaji huo kumaliziwa katika kliniki Cleveland huko Ohio eneo ambalo upandikizaji ndio ulifanyiwa.

Kabla ya upandikizaji ,Katie alifanya upasuaji mara 22 ili kusaidia upandikizwaji huo ufanikiwe.

Yeye pamoja na familia yake hawakujua hatua gani ambazo alikuwa anapaswa kuzipitia ili kila kitu kifanikiwe.

ummaHaki miliki ya pichaIMAGE COPYRIGHTMAGGIE STEBER/NATIONAL GEOGRAPHIC
Image captionMama yake aliwahi kukataa upasuaji wa mtoto wake usitangazwe kwa umma

“Sikujua ni namna gani upandikizwaji wa sura unafanana”,Katie alieleza.wakati wazazi wangu waliposaidia kuelezea kila kitu kwangunilikuwa na shauku kubwa kuwa na uso ambao unavutia tena

Hatimaye mwezi mei mwaka 2017,Katie alifanyiwa upandikizwaji huo kwa kutumia wafadhili wawili ambao walikuwa wamejitokeza mara baada ya kusubiri kwa mwaka mmoja.

Na maamuzi yaliamuliwa kwamba inabidi watumiwe wafadhili wote wawili waliojitokeza kutoa sura ili kuweza kupata muonekano mzuri.

Katie aliweza kufanyiwa upasuaji mara tatu na lengo lilikuwa ni kuweza kuboresha muonekano wa sura.

Bado Katie anasumbuka kwenye kuongea kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mdomo.Katie ataendelea kunywa dawa katika maisha yake yote ili kuweza kupunguza hatari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na upandikizwaji.

Nafasi nyingine

Msichana huyo aliiambia National Geographic kuwa anatarajia kwenda chuo na kuendelea kupata ushauri nasaha.

Vilevile Katie ameonyesha nia ya kutaka kuongea na vijana juu umuhimu wa maisha,thamani ya maisha na suala la kutaka kujiua.

Daktari aliyekuwa anamuhudumia Katie naye pia alisema kwamba ,anatamani Katie arudie kwenye hali yake ya kawaida kama zamani.Akiweza kurudi kwenye hali yake kama zamani basi ataweza kuwa msemaji mzuri katika mambo mbalimbali kwa namna ambavyo amekuwa jasiri .

Comments

comments