Bi. Maria Duhia azungumza na Waandishi wa habari Kuhusu Mavazi.

IMG_0202

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na mmiliki wa kampuni ya mitindo ya Duhia Couture BI.MARIA DUHIA wakati akizungumza na waandishi wa habari.Amesema mavazi yanaonyesha taswira ya MTU alivyo hivyo wanapaswa kuangalia suala hilo kwa umakini.Aidha ameongeza kuwa waislamu na jamii kwa ujumla wanapaswa kufuata maadili ya mtanzania. Kwa upande wa mavazi na kisisitiza kuwa ndio maana ameamua kutengeneza mavazi ya aina hiyo.

IMG_0205

Kwa upande wake mshonaji wa nguo hizo BI.MERY ELIAS amewaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kushona mavazi hayo kwa ajili ya mwezi mtukufu wa ramadhani ili kulinda maadili ya kiislamu.

 

  • Mwandishi :Amina Chekanae
  • Picha : Shyness Mdegela
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments