Benki ya CRDB imemuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA kwenye kampeni

Mkuu wa Mkoa

Benki ya CRDB imemuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA kwenye kampeni ya ujenzi wa ofisi za kisasa za walimu kwa kutoa kiasi cha shilingi Milioni ambapo leo wameanza kwa kukabidhi hundi ya shilingi milioni mia moja.

Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi hiyo Jijini DAR-ES-SALAAM Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB DKT. CHARLES KIMEI amesema wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa ili kusaidia kampeni hiyo kwa lengo la kuwafanya walimu kufanya kazi katika mazingira bora na rafiki na hatimaye kuongeza tija katika ufaulu kwa wanafunzi.

Akipokea hundi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam MAKONDA ameishukuru benki ya CRDB na kusisitiza kuwa fedha hizo zitasaidia kununua mifuko elfu ishirini ya saruji itakayosaidia kufyatua matofali 560,000 ambayo yatajenga ofisi 88 za walimu.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments