Bei ya umeme imepanda kwa asilimia 8.5 kwa mwaka wa 2017

Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) director general, Felix Ngamlagosi speaks to journalist in Dar es Salaam yesterday. Left is Ewura general economist analyst Epheta Ole Lolubo. PHOTO|VENANCE NESTORY

Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini Tanzania (Ewura)  Bw.Felix Ngamlagosi

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji nchini (Ewura) jana imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 8.5 na kupinga ya asilimia 18.19 ambayo ilikuwa ikiombwa na shirika la umeme Tanzania(Tanesco) ambazo gharama hizo zimeonekana zingewaumiza wanachi kulingana na kipato  na kupelekea kupitisha kiasi hicho kitakachoanza kutumika kwa mwaka 2017.

Amesema hayo jana mkurugenzi wa mamlaka wa udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini(Ewura) Bw.Felix Ngamlagosi kuwa awali Tanesco iliwasilisha maombi ya kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18.5 ambayo yalikataliwa na Bodi ya wakurugenzi wa (Ewura) na kuwasilisha tena ombi lingine la ongezeko la bei kutoka shilingi 242.20 hadi kufikia shilingi 286.28 kwa kila unit moja ya umeme sawa na asilimia 18.19.

Aidha mkurugenzi Ngamlagosi amesema pamoja na hayo Tanesco pia iliwasilisha ombi la kuvunja kundi la (TI) na kuligawa katika makundi mawili  yaani TIa ambalo litajumuisha wateja wa majumbani, biashara ndogondogo na taa za barabarani na TIb  litakalohusisha viwanda vidogo,mabango na minara ya mawasiliano ambapo katika kuchambua maoni ya Tanesco mamlaka iliongozwa na sera ya nishati ya  mwaka 2015 sheria ya Ewura sura ya 414 na sheria ya umeme sura namba 131 na kanuni za kurekebisha  bei za umeme ya mwaka 2016 na mwongozo wa bei za uwasilishaji wa maombi ya kurekebisha bei wa Ewura wa mwaka 2009.

Hata hivyo amesema kuwa kutokana na sababu zilizotolewa na  shirika hilo la umeme nchini Tanesco ukilinganisha na maombi ya wadau,EWURA imeridhia na kuwataka Tanesco kuboresha miundo mbinu na  kusema kuwa kutokana na marekebisho yaliyofanyika jumla ya mapato yatakayohitajika kwa mwaka 2017 ni shilingi 1,608.47 bilioni na hivyo kuwa na ongezeko la bei la wastani wa asilimia 8.5 kutoka shilingi 242.34 kwa unit hadi shilingi 263.02 kwa unit.

#SIBUKA MEDIA

#Imeandaliwa na Tuse Kasambala

 

Comments

comments