Bank ya dunia imekabidhi pikpiki 14 kwa ofisi ya takwimu ya taifa

IMG-20170215-WA0006
Bank ya dunia imekabidhi pikpiki 14 kwa ofisi ya takwimu ya taifa zenye zaidi ya thamani ya shilingi milioni 66 ambazo zitatumika katika kuboresha ukusanyaji wa takwimu hapa nchini.
Akikabidhi pikipiki hizo leo mratibu wa uboreshaji wa takwimu kutoka bank ya dunia Bi Nadya Belhaji amesema kuwa pikpiki hizo zitasaidia ofisi ya taifa ya takwimu katika kuongeza ufanisi wa utendaji wa ofisi ya taifa ya takwimu kwa kisaidia ukusaaji wa takwimu.
Bi Belhaji aliongeza kuwa benki ya dunia kwa kutambua umuhimu wa ofisi ya taifa ya Takwimu imetoa msaada huo ili kuiwezesha ofisi hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi. 
IMG-20170215-WA0005
Pia Bi Belhaji aliongeza kuwa benki ya dunia kwa kutambua muhimu wa ofisi ya taifa ya Takwimu imetoa msaada huo ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake.
Aliongeza kuwa pikipiki hizo zigawanywa katika mikoa ya dar es salaam, Kilimanjaro, simiyu, geita, katavi, mwanza, pwani, songwe, njombe na dodoma ili zikasaidie utendaji wa ofisi hiyo. 
Kwa upamde wake mkurugenzi wa ofisi ya taifa ya Takwimu bi agness chuwa 
Alisema ofisi ya taifa ya takwimu ameishukuru benki ya dunia kwa msaada huo kwan umejikita zaidi katika kuiwezesha ofisi yake kutekeleza majukumi yake kwa ufanisi zaidi. 
Pia mkurugenzi huyo amewaasa watumishi kuzitunza pikipiki hizo pamoja na kutumia msaada huo kama ulivyokusudiwa. 
Imeandaliwa na Tuse Kasambala
#SIBUKAMEDIA

Comments

comments