Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya uandishi wa habari, amelalamikia ukosefu wa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field).

Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya uandishi wa habari kikiwemo cha Times school of journalism (TSJ), na Dar es salaam school of journalism (DSJ),vilivyopo ilala Bungoni jijini Dar salaam,wamelalamikia ukosefu wa nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo (field).

Akizungumza na sibuka fm, Mratibu wa masomo kutoka  chuo cha TSJ BI. BLANDINA SEMAGANGA amekiri kuwa idadi kubwa ya wanafunzi hawajapata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo katika vyombo mbalimbali vya habari jambo ambalo litachangia wanafunzi hao kuchelewa kuendelea na muhula ujao wa masomo.

Nae Mratibu wa masomo kutoka chuo cha DSJ, BI. JOYCE MBOGO, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na amewataka wanafunzi wanaopata nafasi kuzitumia vizuri.

Kufuatia changamoto hiyo baadhi ya wanafunzi akiwemo ABDRAKHAN JUMANNE na ALLEN HENJEWELE kutoka chuo cha TSJ na DSJ wamewaomba wamiliki wa vyuo na vyombo vya habari kutafuta ufumbuzi wa haraka ili kufanikisha mazoezi hayo kwa kuwa ni sehemu ya masomo.

Kwa upande wake mhariri mkuu wa gazeti la MIZANI, BW. BADRU YAHAYA amewashauri walimu kubadilisha mfumo wa wanafunzi kufanya mazoezi hayo kwani kwa sasa wanafunzi hao wanafanya mazoezi kwa wakati mmoja.

  • Mwandishi : Amina Chekanae
  • #SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments