Baadhi ya maeneo ya MBEZI MWISHO jijini DAR ES SALAAM yanalalamikiwa na wananchi kuwa na miundombinu mibovu.

FM

Baadhi ya maeneo ya MBEZI MWISHO jijini DAR ES SALAAM  yanalalamikiwa na wananchi kuwa na miundombinu mibovu hasa  barabara ambayo inawapa shida watoto wakati wa kwenda shule.

Akizungumza na SIBUKA FM mmoja wa wakazi wa eneo hilo BI.MAIMUNA ABDALLAH amesema tokea mvua zianze kunyesha hali ya barabara imezidi kuwa mbaya na baadhi ya madaraja yameanguka hivyo kusababisha barabara kushindwa kupitika.

Kufuatia adha hiyo wameiomba serikali kupitia mwenyekiti wa serikali ya mtaa na diwani kushughulikia tatizo hilo kwa haraka zaidi kwa madai kuwa njia hiyo ni kero mvua zinaponyeesha .

SIBUKA FM imefika kwa Mwenyekiti wa mtaa huo BW.OTHMAN CHANDE  ambaye amekiri kuwepo adha hiyo ambapo amesema tayari hatua za mwanzo zimeshaanza kuchukuliwa na muda si mrefu ujenzi  wa daraja utaanza na hali itarudi kama kawaida.

BW.CHANDE ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali ya mtaa huo katika kufanikisha ujenzi wa daraja hilo.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments