Tatizo la wizi wa magari na uvunjaji wa sheria za barabarani limepatiwa ufumbuzi.

Tatizo la wizi wa magari na uvunjaji wa sheria za barabarani limepatiwa ufumbuzi kwa kuanzishwa mfumo mpya wa kuonyesha,kusimamia na kufuatilia vyombo vyombo vya usafiri kwa njia ya mtandao.

Hayo yamebainishwa leo jijini DAR-ES-SALAAM na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa DAR-ES-SALAAM ACP.AWADH HAJI wakati wa kufanya majaribio ya mfumo huo na kuongeza kuwa kupitia mfumo huo madereva wasio na leseni pamoja na ujambazi vitadhibitiwa.

ACP.AWADH amesema kuwa changamoto za ajali za barabarani na makosa ya madereva wanaotumia barabara vimekuwa vikipoteza maisha ya watanzania wengi jambo ambalo kama jeshi la polisi wameona kuwa mfumo huo utakuwa muarobaini wake.

Mapema akitoa maelezo ya namna mfumo huo utakavyofanya kazi Meneja wa kampuni ya TAMOBA SECURITY iliyotengeneza mfumo huo Bwana SALMIN KIONDO amesema mfumo huo umetengenezwa na watanzania kupitia kampuni hiyo na utakapoanza utatengeneza ajira kwa vijana elfu mbili na mia tano ambao watakuwa wakifanya kazi kwenye idara ya Tehama.

 

  • Mwandishi: Stanley Burushi.
  • Mhariri : Amina Chekanae
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments