Watanzania wote bila kujali jinsia,dini wala kabila wameshauriwa kumpongeza Rais Magufuli kwa kupigania Rasilimali za wanyonge na masikini.

WWWWWW

Watanzania wote bila kujali jinsia,dini wala kabila wameshauriwa kumpongeza Rais Magufuli kwa kupigania Rasilimali za wanyonge na masikini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Sengerema kupitia chama cha Mapinduzi( Ccm ) 2015 Bw.Laurence Mabawa ambapo amesema atazunguka nchi nzima kwa gharama zake kuendesha kampeni za “Magufuli Baki”ili kusikiliza maoni ya wananchi endapo Dr.Magufuli abaki pindi atakapomaliza muda wake.

Mabawa amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao hutoa lugha za maudhi na kejeli kwa baadhi ya watanzania wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

Amesema kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 inatoa haki kwa kila mtanzania kutoa maoni yake bila kuvunja katiba kwahiyo kitendo cha kushambuliwa kwa maneno makali ni kosa kisheria.

  • Imeandaliwa na Tuse Kasambala
  • SIBUKA MEDIA

Comments

comments