Amref Tanzania kukutanisha wadau wa Afya nchini ili kutoa mrejesho wa masuala ya Afya

IMG_20170705_204035_460

Waziri wa Afya Mahamood Kombo

Shirika la kimataifa la Amref Tanzania limewakutanisha wadau mbalimbali wa afya katika mkutano wa mwaka ili kutoa mrejesho,changamoto na malengo kupitia miradi ya afya inayofadhiliwa na Amref.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na meneja mawasiliano na uhusiano wa Amref Bi.Eliminata Pasco kuwa nchini Tanzania Amref inashughulika na jumla ya miradi 25 ikiwemo mama na mtoto pamoja na miradi mingine ya malaria,Fistula na mingineyo.

Aidha Bi.Eliminata amesema kuwa Amref imeadhimisha miaka sitini ya utekelezaji shughuli zake ambapo wanatoa huduma takribani nchi 38 Afrika lengo likiwa ni kujenga jamii bora na yenye Afya.

IMG-20170705-WA0034

Wadau wa afya nchini

Nae mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo Waziri wa Afya ,jinsia,wazee na watoto Zanzibar Mahamood Kombo ametoa pongezi kwa Amref Tanzania kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika masuala ya afya.

Mwandishi: Tuse kasambala.

#Sibukamedia

Comments

comments