Aliyewahi kuwa meya wa jiji la DAR ES SALAAM,KLEIST SYKES amefariki dunia.

Aliyewahi kuwa meya wa jiji la DAR ES SALAAM,KLEIST SYKES amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya AGA KHAN jijini DAR ES SALAAM.

KLEIST SYKES aliyehudumu nafasi kuanzia mwaka 2000-2005 amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyikuwa yakimsumbua.

Taarifa za awali kutoka ndani ya familia zimesema mipango ya mazishi inaendelea na tayari ndugu wameshakutana kujua taratibu za mazishi ya kiongozi huyo.

Akizungumza baada ya kupata taarifa hizo meya wa jiji la DAR ES SALAAM,ISAYA MWITA amesema amesikitishwa na taarifa hizo kwani wiki chache zilizopita alimtembelea ofisini kwake na kuzmshauri namna ya kufanya kazi vizuri.

Kwa mujibu wa taarifa za familia marehemu KLEIST SYKES atazikwa kesho tarehe 23 novemba katika makaburi ya kisutu jijini dar es salaam baada ya sala ya alasiri.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN.

  • #SIBUKAMEDIA

 

 

Comments

comments