Ajali yaua mtoto Mkoani KIGOMA.

KIGOMA

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa wilaya ya kasulu mkoani kigoma amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Mitisubishi Kenta lililokuwa likirudi nyuma na kusababisha kifo chake.

Akithibisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani kigoma naibu kamishina FERDNAND MTUI amemtaja mtoto aliyefariki kuwa ni Hans Fikiri aliyegongwa na na gari lililokuwa likiendeshwa na Martin Lulese mwenye umri wa miaka 38.

kamanda  Mtui ameongeza kuwa baada ya ajari hiyo marehemu alipelekwa katika hospitali ya wilaya ya kasulu, hata hivyo alifariki wakati akiendelea kupatiwa matibu huku chanzo cha ajari kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva  wa gari  ambae baada ya tukio hilo ametoweka pasipo julikana huku jeshi la polisi mkoani humo likiendelea na jitihada za kumsaka mtuhumiwa huyo.

Aidha katika tukio lingine kamanda mtui amesema mtoto wa kike anaekadiriwa kuwa na umri wa siku moja ameokotwa akiwa hai baada ya kutelekezwa nje ya kanisa la FPCT lililopo kitongoji cha nyakelela wilyani kasuliu.

Amebainisha kuwa mtoto huyo amechukuliwa na kupelekwa katika hosptali ya nyarugusu wilayani Kasulu kwa ajili ya uangalizi zaidi, wakati juhudi za kumtafuta mtuhumiwa wa tukio zikiendelea, sambamba na kutoa rai kwa wazazi mkoani kigoma kuacha vitendo vya namna hiyo kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai.

  • Mwandishi : Saulo Stephen
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments