Zaidi ya magari 10 yamezuiliwa na askari wa usalama barabarani.

Zaidi ya magari 10 yamezuiliwa na askari wa usalama barabarani ili kufanyiwa ukaguzi .

Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo,jijini DAR ES SALAAM,BW,SAID IBRAHIM amesema magari hayo yaliyozuiliwa yote ni mabovu na kwamba wanayashughulikiwa.

Amesema wamejipanga kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu kwa kupanda mabasi mabovu kwa kuwa wengi wanasafiri na familia zao hivyo ni hatari kutumia usafiri usio na uhakika.

Aidha SUMATRA imewakumbusha wananchi wanaotaka kusafiri wakati huu kupanga safari zao mapema ili kuepusha usumbufu kwa kuwa watu wengi wanasafiri wakati huu wa mwisho wa mwaka.

Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA imetangaza kutoa leseni za muda mfupi ili kusaidia usafiri wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments