Afisa wa tume ya uchaguzi nchini Kenya aliyetoweka apatikana amefariki.

Afisa wa cheo cha juu wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki.

Chris Musando ambaye ni meneja wa masuala ya teknolojia wa IEBC, alipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi

Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS na mmoja wa wafanyakazi wenzake.

Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.

Polisi wanasema kuwa mwili wa afisa huyo pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la kikuyu lililo vitongoji vya mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Bwana Musando alikuwa akihusika na usambazaji wa vifaa vyaa eletroniki ambavyo vingetumiwa kutambua wapiga kura na kwa upeperushaji wa matokeo wakati wa uchaguzi mkuu wiki ijayo.

  • #SIBUKAMEDIA
  • #BBCSWAHILI

Comments

comments