ACT Kufanya tathimini katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika.

ZITTO

KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema wanajipanga kwa kuanza kufanya tathimini ya uchaguzi baada ya kupata taarifa kuwa hawajashinda hata kata moja katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika jana jumapili.

Adiha kiongozi huyo amelaani vitendo vya vurugunna fujo vilivyofanywa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na kusababisha taharuki miongopnmi mwa wapiga kura.

Kiongozi huyo amesema walisimamisha wagombea  17 katika kata zote 43 ambazo hata hivyo hawakupata nafasi kutoka kwa wananchi na kusisitiza kuwa wameyapokea na wameridhika na hali hiyo.

Aidha ZITTO amesema sasa wanajiandaa na chaguzi ndogo zinazokuja ikiwemo za Ubunge kwenye majimbo yaliyowazi ambapo amesema watatumia mafunzo waliyoyapata kwenye chaguzi ndogo hizi kujipanga na chaguzi zinazokuja.

Hata hivyo ZITTO amesisitiza kuwa hawatachoka kuendelea kusambaza sera zetu kwani wanaamini ni bora zaidi na zinazoweza kuleta unafuu kwa wananchi.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments