Mhe EDWARD NGOYAI LOWASSA amesema hana mpango wa kurudi CCM.

LOWASAAAA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambae pia aliwahi  kugombea urais urais kupitia  CHADEMA 2015 EDWARD NGOYAI LOWASSA amesema hana mpango wa kurudi CCM baada ya kukihama chama hicho mwaka 2015.

Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya taarifa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA,MRISHO GAMBO na kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa kiongozi huyo ana mpango wa kurudi CCM kama walivyofanya wanchama wengine wa CHADEMA kurudi CCM.

Kiongozi huyo amewataka wanachama wa CHADEMA kupuuzia kauli hiyo kwa kuwa haina ukweli wowote kwani kwa sasa hafikirii kurudi CCM.

Hivi karibuni MRISHO GAMBO alisikika akisema kwamba amefuatwa na baadhi ya watu ambao wametumwa na LOWASSA, kumuomba amsaidie kukutana na Rais MAGUFULI ili aweze kurejea CCM, kwani uamuzi ambao aliufanya mwaka 2015 wa kuhama chama ulikuwa ni uamuzi wa hasira.

 #SIBUKAMEDIA

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments

comments