Wakazi wa Kata ya KIKOMBO Manispaa ya DODOMA wameiomba serikali na wadau wa sekta ya afya, kusaidia ujenzi wa wodi ya kulaza watoto

Wakazi wa Kata ya KIKOMBO Manispaa ya DODOMA wameiomba serikali na wadau wa sekta ya afya, kusaidia ujenzi wa wodi ya kulaza watoto na chumba cha upasuaji kwenye kituo cha afya cha kata hiyo ili kuondoa  kero ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma afya.

Wakazi hao wametoa kilio hicho wakati wakizungumza na Radio Sibuka Fm katika kijiji cha KIKOMBO kata ya KIKOMBO.

Wamesema kwa sasa inapotokeza dharura ya watoto kulazwa kwa ajili ya oparesheni lazima wasafirishwe mpaka hospitali ya rufaa mjini DODOMA kwa sababu ya kukosa wodi ya watoto.

Wakazi hao wa kata ya KIKOMBO wameongeza kuwa kutokana na tatizo la kukosa wodi wakati mwingine watoto wadogo wanalazimika kulazwa katika wodi za akinamama na akibaba hali ambayo ni hatari kwa watoto.

Aidha wakazi hao wamesema kuwa wapo tayari kshirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa sekta watakaokuwa tayari kusaidia  ujenzi huo wa wodi za watoto na chumba cha upasuaji.

Kwa upande wake mkuu wa kituo cha afya cha KIKOMBO, DKT. JEMES MIRUYE amekiri kituo kukosa  wodi ya watoto na kulazimika kuwachanganya watoto katika wodi za wakubwa pale inatokeza dharura.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments