Mlipuko na kusababisha wanafunzi kupoteza maisha mkoani KAGERA

Siku moja baada ya kutokea mlipuko na kusababisha wanafunzi kupoteza maisha mkoani KAGERA,limeeleza chanzo cha kutokea kwa mlipuko huo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani KAGERA, AGUSTINO OLOMI amesema kuwa chanzo cha wanafunzi kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana na Mwanafunzi kuokota bomu hilo akidhani chuma chakavu.

Kamanda OLOMI amewaambia waandishi wa habari kuwa katika kijiji hicho wakazi wamekua na tabia ya kuokota vyuma kwenda kuuza ili waweze kujipatia fedha ambazo wanazitumia kwa mahitaji mbalimbali.

Amesema tabia hiyo imeenea miongoni mwa wanafunzi ambao wakiokota vyuma hivyo wanavipeleka kwa wanunuzi ambao wanawapatia madaftari au mara chache fedha taslim.

Akithibitisha kuwa chuma hicho kilikuwa ni bomu la mkono, Kamanda wa Kikosi cha kulinda

mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ  Wilaya ya NGARA Meja Jenerali, TR MUTAGUZWA amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari kubwa zaidi.

  •  #SIBUKAMEDIA

Comments

comments