Mkuu wa wilaya Bi. Sophia Mjema leo akikabidhi zawadi za bahati nasibu kutoka SIBUKA LOTTO.

Uongozi wa SIBUKA MEDIA umepongezwa kwa kuanzisha bahati nasibu ya SIBUKA LOTTO ambayo imeanza kubadilisha maisha ya watanzania katika mapambano ya kupiga vita umasikini.

Mkuu wa wilaya ya ILALA, BI. SOPHIA MJEMA ametoa pongezi hizo mapema leo wakati akikabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza na kuongeza kuwa kupitia zawadi hizo washindi wanaweza kujiajiri na hatimaye kukuza kipato.

MJEMA amesema kuwa bahati nasibu hiyo iko tofauti na zingine kwani inatoa vifaa ambavyo mshindi anaweza kuvitumia kujiingizia kipato na kusaidia familia.

IMG_3747

Nao washindi wa bahati nasibu hiyo BI. AMINA CHACHA na BW. EVODI SAMBAGI wameishukuru SIBUKA MEDIA kwa kubadilisha maisha yao na kuwaomba watanzania waendelee kushiriki bahati nasibu hiyo huku wakiahidi kutumia zawadi walizozipata kujikwamua kiuchumi.

Bahati nasibu ya SIBUKA LOTTO iliyoanza wiki iliyopita imeanzishwa na kampuni ya SIBUKA MEDIA ambapo zawadi mbalimbali ikiwemo trekta,baiskeli,mipira ya kiwango cha kimataifa,pampu za kunyunyizia dawa,baiskeli na pikipiki zitatolewa katika droo za kila wiki na droo kubwa itakayochezeshwa tarehe 9 disemba,2017.

  • Mwandishi : Amina Chekanae.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments