Utafiti unaonyesha kuwa katika kila dola moja ambayo serikali inawekeza katika uzazi wa mpango mpaka dola sita zinaweza kuokoa shughuli nyingi za maendeleo zikiwemo kupunguza umasikini,elimu na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza.

2cdfaf3

DAR ES SALAAM:

Utafiti unaonyesha kuwa katika kila dola moja ambayo serikali inawekeza katika uzazi wa mpango mpaka dola sita zinaweza kuokoa shughuli nyingi za maendeleo zikiwemo kupunguza umasikini,elimu na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza.

Hayo yamesemwa katika maadhimisho ya kimataifa ya siku ya idadi ya watu duniani na Kaimu muwakilishi mkazi wa shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani(UNFPA)  Dr.Hashina  Begum kuwa uzazi wa mpango ukizingatiwa Taifa litakuwa katika tija nzuri.

Aidha Dr. Begum amesema kuwa uwekezaji wa uzazi wa mpango ni kuwekeza katika afya pamoja na kuwekeza katika haki za wanawake duniani kote  ambapo husaidia katika kuendeleza uchumi  katika usawa wa kijinsia ili kufikia malengo 17  ya milenia ifikapo mwaka 2030.

Begum amesema kuwa maadhimisho hayo yanaadhimishwa sambamba na mkutano wa kimataifa unaofanyika London  malengo ya uzazi wa mpango kuelekea mwaka 2020 ambayo yamekusudiwa kupanua uzazi wa mpango  kwa wanawake.

Nae kaimu katibu mkuu wizara ya afya,maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Bi Otilia Gowele akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya Dr.Kigwangala amesema kuwa serikali imeimarisha huduma za afya ya uzazi ili kukabiliana na ongezeko la watu pasipo tija.

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani hufanyika kila mwaka tarehe 11 mwezi wa saba ambapo Kaulimbiu ya mwaka 2017 ni “Uzazi wa Mpango kuwezesha watu na kuendeleza Mataifa

#imeandaliwa na Tuse Kasambala

#Sibuka Media

Comments

comments