Iyumbu Manispaa ya Dodoma hatimaye Kuondokana na adha ya kusafiri

DODOOO

Wakazi wa kijiji cha Iyumbu manispaa ya Dodoma hatimaye wameondokana na adha ya kusafiri umbali wa zaidi ya kilometa 15 kufuata huduma za afya baada ya wadau wa maendeleo kukabidhi zahanati ya kisasa ambayo itahudumia wagonjwa kijijini hapo na maeneo ya jirani hali itakayosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto

Huduma ya Afya ni moja ya kipaumbele muhimu katika kujenga taifa imara ambapo katika baadhi ya maeneo hapa nchini kumekuwa na changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya Afya na mara nyingine umbali mrefu umekuwa ukisababisha vifo vya mama na mtoto

Wakizungumza katika makabidhiano hayo baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wanasema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilazimika kusafiri mpaka hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kufuata huduma za afya hali iliyokuwa ikichangia wagonjwa wengi kufariki dunia hasa wajawazito.

Mmoja wa wafadhili wa mradi huo wa Zahanati anasema kuwa wameguswa na matatizo yanaikabili eneo la Iyumbu na licha ya kituoa cha Afya pia wadau hao wamechimba visima vitatu vya maji ili kuwapatia wananchi maji safi na salama

Nae mbunge wa jimbo la Dodoma mjini ambaye pia  ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu sera bunge ajira na vijana  Anthony Mavunde ambaye ameongoza zoezi la makabidhiano ya zahanati hiyo amewataka viongozi na wakazi wa eneo hilo kuhakikisha zahanati hiyo inatuzwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo pamoja na kutoa huduma bila upendeleo.

Mwito unatolewa kwa wadau wengine wa maendeleo kuwa na uzalendo katika kusaidia jamii kupata huduma muhimu ikiwemo miundombinu ya barabara,huduma za maji safi na salama pamoja na sekta za Afya na hatimaye kulipeka taifa katika uchumi wa kati

Imeandaliwa na Barnaba Kisengi

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments