Tafiti zilizotolewa na Bank kuu ya dunia kupitia delivery Indicators Kuhusu Walimu Kutokuwa Darasani wakati wa Masomo

DSC_0572

Tafiti zilizotolewa na bank kuu ya dunia kupitia delivery indicators imeonyesha kuwa 37% ya waalimu waliokutwa mashuleni hawakuwa madarasani katika muda wa masomo hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya elimu nchini

Amesema hayo leo mkurugenzi mtendaji wa ECONNECT Bwn Hashimu Magesa alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam leo,ambapo amesema kuwa jambo hilo la kukosekana kwa waalimu madarasani katika muda wa masomo linaashiria kuwa wanafunzi hawapati elimu kwa kiwango kilichokusudiwa na wizara ya elimu na mamlaka yake

Ameongeza kuwa pamoja na changamoto hizo za waalimu kumekuwepo na wanafunzi hewa pamoja na utoro uliopitiliza  hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya elimu kwa kutokujua kusoma na kuandika

Aidha Bwn Magese amesema kuwa kutokana na changamoto hizo na nyinginezo zinazoikabioli sekta ya elimu hapa nchini ndio maana taasisi ya ECONNECT imekuja  na mfumo huo wa Kanzidata utakao isadia serikali kutatua changamoto za kielimu kwa ujumla

Amesema kuwa mfumo huo wa Kanzidata(DATABASE)utasaidia kuwa na takwim u sahihi zinazohusu kujua idadi shule,waalimu,wanafunzi,madarasa,madawati nk pamoja na mkwamo wa mawasiliano kati ya utawala wa shule na mzazi/mlezi utakaokuwa ukitoa taarifa kwa haraka juu ya maendeleo ya haki elimu kwa mwanafunzi kupitia mawasiliano ya simu za kiganjano ambao utagarimu shilingi mia tatu kwa ajili ya kupata huduma zote hizo

Bwn Magesa amesema kutokana na utafiti wa majaribio walioufanya kwenye wilaya ya ilala kwa jumla ya shule 152 ampo katika zoezi hilo waliorodhesha taarifa mbalimbali za kielimu kupitia takwimu sahihi ambazo kwa sasa zinawapa taarifa na kuokoa fedha ambazo zingetumika kuchapisha taarifa na huku taarifa hizo zikifika kwa haraka kwa wahusika

Hata hivyo taasisi ya ECONNECT imetoa wito kwa serikali kuutumia mfumo wa majaribio kwa ndani ya mwaka mmoja ili kujiridhisha na ufanisi wake,pia taasisi inawataka wadau mbali mbali wa elimu ikiwa ni pamoja na makampuni,taasisi na watu binafsi kushirikiana kwa pamoja kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa mfumo utakaosadia kuboresha elimu hapa nchini kwa manufaa ya taifa letu kwa ujumla.
Imeandaliwa na Tuse Kasambala.
#SIBUKAMEDIA

Comments

comments