Ziara Ya Waziri wa China WANG Yi Nchini Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, Mh. WANG Yi Akiwa na mwenyeji wake Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Mh. Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, Mh. WANG Yi Akiwa na mwenyeji wake Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa  Afrika Mashariki, Mh. Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Waziri wa mambo ya nje wa jamhuri ya watu wa china Mhe.Wang Yi jana amewasili jijini Dar es salaam nchini Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Mhe. Dkt. Augustine Maige na kuweza kufanya makubaliano ambayo yataendeleza uhusiano uliyopo baina ya nchi hizo mbili za Tanzania na China ambao umedumu  zaidi ya miaka 50.

Akizungumza na waandishi wa  habari  katika ukumbi wa JKICC Mhe. Balozi Maige amesema kuwa lengo la Mh.Wang YI ni kuwakilisha jamhuri ya China katika kutiliana mikataba ambayo  nchi ya China inategemea kujenga viwanda nchini Tanzania visivopungua 200 pamoja na kuhamishia baaadhi ya viwanda nchini.

Ameongeza kuwa  kwa pamoja pia wanatarajia kujenga bandari ya Bagamoyo,kuimarish viwanja vya Zanzibar.

Nae Waziri.Wang YI amesema kuwa ana imani kubwa na serikali ya Tanzania kwakuwa imekuwa ni nchi yenye amani na utulivu hivyo kwa pamoja watakuza uchumi wa nchi hizo mbili.

Imeandaliwa na Tuse Kasambala.

#Sibukamedia

 

Comments

comments