Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Leo Ametimiza ahadi yake ya kutoa Msaada

makonda-4

Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam Paul Makonda leo ametimiza ahadi yake ya kutoa msaada na zawadi kwa makundi mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa katika ziara yake ya siku kumi aliyoifanya mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa akiwa na wanaostahili kupokea zawadi hizo Makonda amesema kuwa wakati wa ziara yake aliona mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuona namna ambavyo baadhi ya watumishi wa serikali katika mkoa wake wanavyofanya kazi katika mazingira magumu na hivyo kuona umuhimu wa kufanya jambo.makonda-5

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa zawadi kwa watumishi wane ambao utendaji wao wa kazi umedhihirisha ari yao ya utayari wa kujitolea kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu ambapo watumishi waliopata zawadi hizo ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Dkt.Grace Magembe,Kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke Kamishna Mroto,Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji sekretarieti ya Mkoa Bwana Edward Otieno na Mkurugenzi wa Uendeshaji DAWASCO makao makuu Bwana Aron Joseph.

Zawadi zilizotolewa ni pamoja na pikipiki,televisheni,mabati,jiko la gesi,kingamuzi,magodoro,friji pamoja na gari la kubebea wagonjwa kwa kikosi cha FFU Ukonga huku thamani halisi ya vifaa hivyo ikiwa ni shilingi 164,272,000/=

#SIBUKA MEDIA

#Imeandaliwa na Stanley Burushi

 

Comments

comments